RicMwambe

Richard R. Mwambe, Mwandishi na mtunzi wa riwaya za Kisawahili. Ni Mtanzania kutoka mkoa wa Lindi. Ni Msanii wa sanaa ya jukwaani, Mtengeneza filamu, Mwandishi wa script na Muongozaji filam. Mtunzi na mwandishi wa kitabu - TUFAA JEKUNDU. Licha ya kazi ya sanaa yeye ni fundi Umeme daraja la kwanza pia ni fundi wa kompyuta (IT). Na ni dereva wa gari mwenye uzoefu na weledi mkubwa. Elimu: Amepata Elimu yake ya Msingi amepata katika shule ya Msingi Ukonga mwaka 1988 - 1984. Kisha akajiunga na Chuo cha Ufundi Dar Tech 1995- 1997 na kutunukiwa cheti cha General Course in Engineering (GCE). Mwaka 2001-2004 alijiunga na VETA Dar es salaam na kutunukiwa cheti cha ufundi stadi wa umeme daraja la kwanza. Amepata elimu yake ya ufundi wa kompyuta katika Chuo Kikuu cha Ruaha-Iringa (RUCO) chini ya kozi za SISCO mwaka 2010-2011, Kipaji chake cha kuzaliwa cha sanaa amekiongezea nguvu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo mwaka 2014... mpaka sasa. Pia amefanya kozi nyingi fupi katika nyanja za Uhifadhi Misitu -TaTEDo IT na Informatics - DREAM Mult Skill (Entepreneurship) - Soft Trainers Usalama Barabarani - APEC na Jeshi la Polisi Dodoma Uongozaji Muziki na Uimbaji - TaSUBa na Taasisi ya Muziki Ujerumani Uzoefu wa Kazi: Amefanya kazi katika kampuni/miradi tofauti. UNIBILT (T) LTD - Dar es salaam - kama fundi na mwendesha mitambo Project Vincenza - Iringa - kama fundi wa vifaa tiba DREAM program - Iringa - kama fundi umeme, IT na dereva Piero Pasolini Hydroelectric Power Station - Cameroon- kama fundi umeme Nchi alizotembelea Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia, Cameroon Imani Ni Mkristo wa kanisa Katoliki pia ni mfuasi wa Movement ya Focolare Licha ya kazi hizo zote, Richard yupo tayari kukupa msaada wa ushauri Kiroho, Maisha, Ndoa na Mapenzi. Karibu, wasiliana naye sasa, +255 766 974865 "Baba wote wawe na umoja..." Yoh 19:21

Posts by RicMwambe

KAA TAYARI KWA TUKIO KUBWA …

#MjueMtunzi Mapicha ya kutisha, kila mmoja akitaraji tukio kubwa Tanzania… #MjueMtunzi ndiyo homa ya jiji kwa sasa. Mimi nataka kumjua mtunzi, wewe je? Kwa abari mbalimbali za #MjueMtunzi, tembelea kurasa zetu Facebook Page: Mjuemtunzi Instagram: mjuemtunzi Tweeter: MjueMtunzi Usipitwe….

Share

The ESCROW MISSION – Riwaya

The ESCROW Mission © Richard R. MWAMBE         1 … Dar es salaam – saa 04:10 MJI WA DAR ES SALAAM uligubikwa na moshi mzito wa mabomu ya machozi, mabomu yaliyokuwa yakirushwa na vijana wakakamavu wa fanya fujo uone ‘FFU’. Vijana wenye uchungu na hasira, macho yao yaliyojaa machozi na makamasi membamba
+ Read More

Share

ZANZIBAR 2017 – Habari Picha

Mwaka 2017, Maisha Film Lab PICHA                    

Share

KITISHO

KITISHO ! Richard MWAMBE     SURA YA 1 Mbowe Club Saa 1:23 usiku RADI kali ilipasua anga na kufanya mchoro wa kutisha, mwanga wake ulilipoteza giza kwa sekunde kadhaa, kila kilichojificha kilionekana wazi. Hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa nje muda huo. Ni mvua kubwa na ngurumo za kutisha zilitawala kila kona, ilikuwa ni hali
+ Read More

Share

RIWAYA: JIUE MWENYEWE

         JIUE  MWENYEWE ©Richard R. MWAMBE   1 Mwaka 2003… DURBAN – AFRIKA KUSINI-Saa 3:21 asubuhi NDANI YA JENGO REFU KULIKO YOTE, Monte Blanc, lililopo katika jiji la Durban, jimbo la KwaZulu Natal, Afrika ya Kusini, ni mtu mmoja aliyekuwa akiwindwa kwa udi na uvumba. Ni mara ya sita kama si tano
+ Read More

Share

PASIPOTI YA GAIDI -Part I – Hujuma na Uzandiki ‘Trailer’

                PASIPOTI YA GAIDI I   hujuma na uzandiki               SURA YA I IKULU – DAR ES SALAAM Saa 10:30 alfajiri WAKATI GIZA LIKIJIANDAA KUTOWEKA na kuipisha nuru ya asubuhi, miti yote ilikuwa imetulia kana kwamba kuna aliyeiambia ifanye hivyo. Ni Tausi
+ Read More

Share

Protected: PASIPOTI YA GAIDI – Part I – Hujuma na Uzandiki

There is no excerpt because this is a protected post.

Share

MAGNUM 22 – official trailer

      I   SEHEMU FULANI HUKO AFRIKA MAGAHARIBI MACHO YANGU yalikuwa mazito sana kiasi kwamba iliniwia ngumu kuyafumbua. Haikuwa rahisi kwangu, nilijaribu kutumia nguvu ya mwisho niliyonayo kuona japo nuru, haikuwezekana. Fahamu zilipokaa sawa nikahisi maumivu makali sana kisogoni, nikajaribu kuinua mkono ili japo kushika eneo hilo la mwili. Damu! Damu iliyoanza kuganda
+ Read More

Share

Protected: MAGNUM 22 – Riwaya Tsh 6,000

There is no excerpt because this is a protected post.

Share
Translate »
error: OPS! Content is protected !! Imezuiwa